Naibu waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo, amefanya ziara kwenye shule mbalimbali mjini Dodoma kuangalia maandalizi kwa ajili ya mtihani wa kidato cha nne unaoanza Leo nchini.
Katika ziara yake kwenye Shule ya sekondari Jamhuri, Kiwanja cha ndege na Msalato, Jafo amewaonya walimu na wanafunzi hao nchini kuepukana na vitendo vya udanganyifu.
Akizungumza na walimu na wanafunzi katika shule hizo, Jafo amesema katika mtihani huo hawatarajii kuwepo na udanganyifu kwa kuwa wamejifunza kupitia mtihani wa darasa la saba ambapo kumekuwepo na tabia ya walimu kujificha chooni ili kuwasaidia wanafunzi.
Amesema shule zitakazofanya fanya hivyo zitakuwa zimepoteza thamani yake.
Ameeleza hatarajii mitihani hiyo ifanyike kinyume na kuwataka walimu wasisubutu kufanya udanganyifu wowote na kuziingiza shule zao kwenye kashfa.
Jafo ame sema mara nyingi mitihani hiyo inapofanyika kumekuwa na wizi wa mitihani na kutofuatwa kwa taratibu za mitihani.
Akizungumza na wanafunzi, Jafo amewataka kujiepusha na vitendo hivyo kwa kuwa vitawafanya wafutiwe mitihani na kupoteza malengo yao kwenye maisha.
Hata hivyo amewahakikishia walimu kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga kuboresha mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia na kuwataka kuwajibika ipasavyo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni