Yaya Toure amerejea kwa kishindo
uwanjani kwa kuifungia Manchester City magoli mawili na kuipatia
ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Crystal Palace.
Toure, akicheza kwa mara ya kwanza
katika ligi kuu ya Uingereza kwa msimu huu baada ya kumaliza tofauti
zake na kocha, alishirikiana vyema na Nolito na kufunga goli la
kwanza.
Hata hivyo Crystal Palace walijibu
mapigo na alikuwa Wilfried Zaha aliyemtengenezea nafasi Connor
Wickham aliyetokea benchi na kusawazisha goli.
Hata hivyo Toure, ambaye hakuwa na
City kwa takriban miezi mitatu alipachika goli la pili akiutumbukiza
kimiani mpira wa kona uliopigwa na Kevin de Bruyne.
Yaya Toure akishangilia goli baada ya kutikisa wavu wa Crystal Palace
Connor Wickham akifunga goli pekee la Crystal Palace katika mchezo huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni