Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Cuba Bwana Fidel Castro kwenye ubalozi wa Cuba Mtaa wa Namanga Mjini Dar es salaam. Kushoto yas Balozi Seif aliyesimama ni Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Bwana Jorge Luis Lopez.
Balozi Seif akitia saini kitabu hicho akishuhudiwa na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Harus Said Suleiman pamoja na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma Nhunga.
Balozi Seif Ali Iddi wa Pili kutoka Kushoto akimfariji Balozi wa Cuba Nchini Tanzania wa kwanza kutoka kushoto mara baada ya kutia saini Kitabu cha maombolezo ya Kifo cha Rais Mstaafu wa Cuba Bwana Fidel Castro.
Balozi wa Cuba Bwana Jorge Luis Lopez akiagwa na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Harus Said Suleiman baada ya kumalizika kwa kazi ya utiaji saini.
Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma Nhunga 023 ni:- Balozi wa Cuba Bwana Jorge Luis Lopez akiagwa na Naibu Waziri wa baada ya kumalizika kwa kazi ya utiaji saini.
Picha na – OMPR – ZNZ.Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametia saini Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Watu wa Cuba Marehemu Fidel Alejandro Castro Ruz kilichotokea Tarehe 25 Novemba 2016 katika Mji wa Biran Nchini Cuba.
Utiaji saini huo wa Kitabu cha Maombolezo ameufanya katika Makaazi ya Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa Cuba Nchini Tanzania uliopo Bara bara ya Ali Bin Said Mtaa wa Namanga Jijini Dar es salaam.
Balozi Seif ameiwakilisha Serikali ya Mainduzi ya Zanzibar katika utiaji saini huo akiambatana na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Harus Said Suleiman , Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma Nhunga pamoja na Mratibu Mkuu wa Ofisi ya Uratibu wa shughuli za SMZ Dar es salaam Nd. Issa Mlingoti Ali.
Marehemu Fidel Alejandro Castro Ruz aliyefikia umri wa Miaka 90 alifanikiwa kuiongoza Jamuhuri ya Cuba akiwa na umri wa Miaka`32 kuanzia mwaka 1959 baada ya vugu vugu la kampeni ya kuuondosha Madarakani utawala wa Batista mwaka 1958 akisaidiwa na Kaka Yake Raul Castro pamoja na mwana harakati wa kupigania ukombozi wa wanyonge Kamanda Guavara.
Akimfariji Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa Cuba Bwana Jorge Luis Loez baada ya saini hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Kifo cha Jemedari huyo wa Taifa la Cuba hakikuacha pengo kwa nchi hiyo lakini pia kimeigusa Tanzania kutokana na Mataifa hayo kufanana katika harakati zao za kupigania Uhuru kutoka makucha ya Kikoloni.
Balozi Seif alisema Jamuhuri ya Cuba ni kaka wa Tanzania katika njia ya kusaidia maendeleo na nyanja za uchumi zilizopata ufanisi mkubwa kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Wataalamu wa Nchi hiyo kuwawezesha Kitaaluma wananchi Wazalendo wa Tanzania.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kupitia Balozi huyo wa Cuba Nchini Tanzania amewataka Wananchi wa Taifa hilo lilioko katika Bahari ya Carribean kukubali kuwa na moyo wa subra katika kipindi hichi cha kuondokewa na Kipenzi Rais wao Mstaafu Kamanda Fidel Castro.
Akitoa shukrani zake Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa Cuba Nchini Tanzania Bwana Jorge Luis Lopez alisema Cuba itaendele kuwa mshirika mkubwa wa Tanzania katika azma yake ya kuona wananchi waliowengi wa ngazi ya chini wa Mataifa hayo wanafaidika na Uhuru walioupata kutoka katika makucha ya wakoloni.
Balozi Lopez alisema Cuba na Tanzania zimeshirikiana kwa muda mrefu uliobakia kuwa Historia kwa sasa hasa katika sekta za Afya, Kilimo, Viwanda na masomo ya Elimu ya Juu, ushirikiano uliowekwa msingi wake na Waasisi wa Nchi hizo Mbili Marehemu Mwalimu Julius K. Nyerere na Bwana Fidel Castro.
Marehemu Fidel Castro alizaliwa Mnamo Tarehe 13 Agosti mwaka 1926 ndani ya familia ya watoto Sita akiwa watatu wa Mzee Angel aliyekuwa mfanyakazi wa mashamba ya miwa akiwa na asili ya Taifa la Hispania.
Marehemu Fidel Castro katika utoto wake alionyesha kipawa chake wakati alipoanza kupata elimu iliyomuwezesha kuonekana mwenye akili kubwa katika masomo yake Darasani tokea maandalizi,msingi, sekondari hadi chuo Kikuu.
Alipohitimu masomo yake katika Chuo Kikuu cha El Colegio de Belen Mjini Havana Nchini Cuba Marehemu Fidel Castro aliamua kujiunga katika harakati za Kisiasa zilizompelekea kukumbwa na misuko suko kadhaa iliyomsababishia kuikimbia Cuba katika miaka ya 40.
Alirejea Nchini Cuba Disemba 2 mwaka 1956 akiambatana na zaidi ya askari 80 wakiwa na silaha kwa ajili ya mapambano lakini nguvu za Kijeshi za Batista zilisababisha kushindwa kwa jeshi hilo na hatimae Castro, Raul, Guavara na baadhi ya askari wao waliamua kukimbilia katika milima ya Sierra Maestra.
Miaka miwili baadaye Marehemu Castrol alijiimarisha tena kijeshi kwa lengo la kupambana kwa mara nyengine na Serikali iliyokuwa ikiongozwa na Batista ambapo mwanzoni mwa mwaka 1958 akaanza kampeni ya kujipenyeza tena Nchini Cuba.
Mbinu za kuimarisha majimbo sambamba na kuyashawishi makampuni ya Kilimo na Viwanda kumkubali zilimuwezesha Castrol na washirika wake kuongeza nguvu zilizoisambatarisha Serikali ya Batista iliyokosa nguvu za kiutawala na hatimae Jeshi la Castrol likafanikiwa kuidhibiti Cuba Kijeshi.
Mwezi Januari mwaka 1959 Batista aliamua kukimbilia Jamuhuri ya Dominica baada ya Serikali yake kushindwa nguvu na Kikosi cha Castrol akisaidiwa na Kaka yake Raul na Mwanaharakati za kupigania uhuru wa wanyonge Kamanda Enersto Guavara.
Bwana Fidel Castro alilazimika kukasimu madaraka kwa kumteuwa Kaka yake Raul Castro mnamo Tarehe 31 Julai 2006 kukaimu nafasi hiyo baada ya afya yake kutomruhusu kuendelea kushika wadhifa wa Urais wa Cuba.
Tarehe 24 Febuari mwaka 2008 Bwana Raul akashika rasmi nafasi hiyo ya Urais na kuendelea kuliongoza Taifa hilo hadi hivi sasa.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
2/12/2016.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni