.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 15 Desemba 2016

BALOZI WA UJERUMANI AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA FEDHA NA KUAHIDI KUJENGWA KWA KIWANDA KIKUBWA CHA MBOLEA MKOANI LINDI

ujeru
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bw. Egon Kochanke (katikati) pamoja na ujumbe wake wakisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani), Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.
ujeru-1
Ujumbe wa Ujerumani ukiongozwa na Balozi wan chi hiyo nchini Tanzania, Egon Kochanke (katikati) ukiwa katika mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Kulia) wakati wa mazungumzo kuhusu uhusiano uliopo kati ya nchi hizo mbili, Jijini Dar es salaam. Kulia kwa Balozi ni Mkurugenzi wa Ushirikiano Bi. Julia Hannig na na kushoto kwake ameketi Naibu Balozi wa Ujerumani hapa nchini Bw. John Reyels.
ujeru-2
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia) akiangalia nyaraka alizokabidhiwa na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bw. Egon Kochankewakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam. Kulia kwa Waziri ni Mchumi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Melckzedek Mbise na anayefuata ni katibu wa Waziri Bw. Makamba.
ujeru-3
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bw. Egon Konchanke akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam.
ujeru-4
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) (wa pili kushoto) akielezea namna ya ushirikiano wa maendeleo kati ya nchi ya Tanzania na Ujerumani unavyoweza kuwa na tija kwa pande zote, wakati wa kikao kati yake na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bw. Egon Konchanke, Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es salaam.
ujeru-5
Mkurugenzi wa ushirikiano kutoka ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bi. Julia Hannig, akifafanua jambo wakati wa kikao kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Egon Kochanke (kulia), Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
ujeru-6
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akiagana na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bw. Egon Kochanke (kulia) baada ya kumalizika kwa kikao kati yao, kilichofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
ujeru-7
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia) akiagana na Mkurugenzi wa Ushirikiano kutoka Ujerumani, Bi. Julia Hannig, nje ya Makao makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango baada ya kumalizika kwa mkutano katika ya ujumbe huo kutoka Ujerumani ukiongozwa na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Egon Kochanke, Jijini Dar es salaam.

                           (Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Hazina)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni