.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 15 Desemba 2016

ZAIDI YA WANATASNIA 200 WA FILAMU WANUFAIKA NA MAFUNZO MAALUMU YA FILAMU MKOANI MARA.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.Nuru Millao (kulia), akifungua warsha (mafunzo) ya siku tatu kwa wanatasnia ya Filamu na Maigizo mkoani Mara, yaliyoanza hii leo (Disemba 14, 2016) katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Mara iliyopo Musoma Mjini.

Wengine ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fissoo (katikati) pamoja na Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba (kushoto).

Warsha hiyo imeandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Bodi ya Filamu nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo wanatasnia ya filamu na maigizo ili kuzalisha kazi zenye ubora (maudhui) na kuboresha soko la ndani na nje ya nchini, kama kaulimbiu isemavyo, "Filamu ni Uchumi, Filamu ni Ajira".

Tayari warsha za aina hiyo zimefanika mikoa ya Morogoro na Mwanza ambapo pia zitaendelea kufanyika katika mikoa mingine nchini ikiwa ni utekelezaji wa kauli ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Nape Nnauye, kuhakikisha wizara hiyo inafikisha huduma zake mikoani badala 
ya Dar es salaam pekee. Na BMG
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fissoo (kushoto) akizungumza kwenye warsha hiyo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.Nuru Millao
Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba akizungumza kwenye warsha hiyo. Katikati ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini Bi.Joyce Fissoo na Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.Nuru Millao
Wanatasnia ya Filamu na Maigizo mkoani Mara, wakimsikiliza Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba wakati akizungumza kwenye warsha ya mafunzo ya filamu kwa wanatasnia hao hii leo.
Kaimu Afisa Utamaduni mkoani Mara, Sheikudadi Saidi, akizungumza kwenye warsha kwa wanatasnia ya filamu na maigizo mkoani Mara, hii leo.
Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaa, idara ya Sanaa, Richard Ndunguru, akitoa semina masuala ya picha nyogevu na uongozaji wa filamu.
Wanatasnia ya Filamu na Maigizo mkoani Mara, wakifuatilia mafunzo kutoka kwa Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaa, idara ya Sanaa, Richard Ndunguru.
Zaidi ya wanatasnia 200 wa Filamu na Maigizo mkoani Mara wamepatiwa mafunzo ya filamu na maigizo kutoka Bodi ya Filamu nchini. Pia wawakilishi kutoka maeneo jirani ikiwemo Simiyu wamehudhuria mafunzo hayo.
Zaidi ya wanatasnia 200 wa Filamu na Maigizo mkoani Mara wamepatiwa mafunzo ya filamu na maigizo kutoka Bodi ya Filamu nchini.
Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuhusiana na umuhimu wa mafunzo hayo katika kuinua tasnia ya filamu na maigizo nchini.
Katibu wa Chama cha Waigizaji mkoani Mara TDFAA, Johnson Ibambai (Dunia), akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) juu ya umuhimu wa mafunzo hayo.
Msemaji wa Chama cha Waigizaji wilayani Bunda, Jaqueline Frank (kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) na kuipongeza serikali kupitia Bodi ya Filamu nchini kwa kutoa mafunzo kwa wanatasnia ya filamu na maigizo ili kuboresha zaidi kazi zao za sanaa.  #BMGHabari
 

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Bodi ya Filamu nchini, imeendelea kuhakikisha inawafikia wanatasinia wa filamu na maigizo nchini na kuwapatia mafunzo kwa ajili ya kuboresha kazi zao.

Akifungua hii leo mafunzo ya siku tatu kwa wanatasinia ya filamu na maigizo mkoani Mara, Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Bi.Nuru Millao, amesema ni vyema mafunzo hayo yakawa chachu ya uboreshaji wa filamu zinazozalishwa nchini na hivyo kuingia kwenye soko la ushindani ndani na nje ya nchi.

Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fissoo, amesema Serikali inayo dhamira ya dhati ya kuhakikisha uchumi wa kati wa viwanda unafikiwa kupitia filamu ndiyo maana imeamua kutoa mafunzo hayo ambayo yatazalisha waigizaji, waongozaji na waandishi bora wa filamu nchini ambao kupitia kazi zao watakuza kipato chao na pato la taifa kwa ujumla.

Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, amesisitiza kwamba filamu ni uchumi, ni ajira na ndiyo maana serikali imeamua kuirasimisha ambapo ameishukuru serikali kwa kufikisha mafunzo hayo hadi ngazi za mikoani.

Zaidi ya wanatasnia 200 wa Filamu na Maigizo mkoani Mara wamepatiwa mafunzo hayo ya filamu na maigizo kupitia Bodi ya Filamu nchini ambapo wamefurahishwa nayo na kuahidi kuyatumia kuboresha kazi zao ikiwemo kuzalisha filamu na vipindi vya luninga vyenye maudhui bora.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni