Timu ya Taifa ya mpira wa miguu unaochezwa ufukweni (Beach Soccer), kesho Ijumaa Novemba 9, 2016 inatarajiwa kucheza na Uganda katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Viwanja vya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ni maandalizi kwa timu Tanzania na Uganda kujiandaa na michuano ijayo ya kimataifa ndani ya bara la Afrika na ile la CAF. TFF inatangaza kuwa mchezo huo hautakuwa na kiingilio.
Waamuzi wa mchezo huo watakuwa Jackson Msilombo, Kessy Ngao, Heri Sassii na mtunza muda anatarajiwa kuwa Idd Maganga.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Beach Soccer, John Mwansasu anatambia nyota wake 12 wakiwamo makipa Rajab Galla na Khalifa Mgaya.
Mabeki ni Roland Revocatus, Juma Ibrahim, Kashiru Salum na Mohammed Rajab wakati Viungo ni Mwalimu Akida, Ahmada Ali na Samwel John huku washambuliaji wengine wakiwa ni Kassim Kilungo na Talib Ally pamoja na Ally Rabbi ambaye ni Nahodha na Mshambulaji wa timu hiyo.
Hivi karibuni kikosi hiki kilicheza na Ivory Coast katika michezo miwili ya kuwania nafasi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa yAfrika kwa soka la ufukweni bila mafanikio.
NUSU FAINALI LIGI YA TFFU20
Nusu fainali ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20, inafanyika kesho Novemba 9, kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Mbagala-nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Hatua hiyo itazikutanisha timu za Azam FC ya Dar es Salaam na Mtibwa Sugar ya Dar es Salaam katika mchezo utakaoanza saa 10.00 (16h00) kabla ya nusu fainali ya pili itazikutanisha timu za Simba ya Dar es Salaam na Stand United ya Shinyanga katika mchezo utakaofanyika kuanzia saa 1.00 )usiku (19h00).
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
http://www.tff.or.tz/news/711-nusu-fainali-ligi-ya-tffu20
HAYATOU WA CAF ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA ISMAIL HALFAN
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (TFF), Bw. Issa Hayatou ametuma salamu za rambirambi kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Jamal Emil Malinzi kutokana na kifo cha ghafla cha Mchezaji Ismail Mrisho Khalfan wa timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 wa Mbao FC ya Mwanza.
“Tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mchezaji Ismail Mrisho Khalfan akiwa na umri mdogo wa miaka 19 baada ya kuzimia katika mchezo wa Ligi ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20,” ilisema sehemu ya barua hiyo ya Rais Hayatou kwenda kwa Rais Malinzi.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
http://www.tff.or.tz/news/710-hayatou-wa-caf-atuma-salamu-za-rambirambi-kifo-cha-ismail-khalfan

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni