Timu ya Taifa ya mpira wa miguu unaochezwa ufukweni (Beach Soccer) ya Tanzania imeifunga Uganda mabao 7-5 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika leo Ijumaa Desemba 9, 2016 kwenye Viwanja vya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na Jackson Msilombo, Kessy Ngao, Heri Sassii na mtunza muda, Idd Maganga mabao ya Tanzania yalifungwa na Samwel Opanga aliyefunga la kwanza, la sita na saba wakati mengine yalifungwa na Kashiru Salum, Ally Babby na Ahmada Abdi aliyefunga mawili.
Mabao ya Uganda yalifungwa na Emma Kalyowa aliyefunga bao la kwanza na la tatu wakati mengine walifungwa na David Kassa, Naturinda Ambrosse na Ochero Sulaimani.
Mchezo huo unaotambuliwa na CAF na FIFA, uliovutia mashabiki wengi wakiongozwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ulilenga kuziandaa timu hizo kujiandaa na michuano ijayo ya kimataifa ndani ya bara la Afrika na ile la CAF.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Beach Soccer, John Mwansasu amesema huu ni mwanzo mzuri wa kuiandaa timu yake na kufikia mafanikio ya juu katika soka la ufukweni hivyo kuwaomba wadau kuzidi kuwaunga mkono.
Hivi karibuni kikosi hiki kilicheza na Ivory Coast katika michezo miwili ya kuwania nafasi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa soka la ufukweni bila mafanikio.
MCHEZO WA KIRAFIKI KUCHANGIA RAMBIRAMBI MSIBA WA ISMAIL KHAFLAN
Kesho Jumamosi Desemba 10, 2016 kutakuwa na mchezo maalumu wa kirafiki utakaozikutanisha timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara Mbao FC na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Mchezo huo utakaoanza saa 10.00 jioni utakuwa ni maalumu kwa ajili ya kutoa heshima kwa marehemu Ismail Khalfan - mchezaji wa timu ya vijana Mbao aliyefariki dunia Desemba 4, mwaka huu wakati akiiitumikia timu yake ya vijana kwenye mchezo wa Ligi ya Vijana ya TFF U20 dhidi ya Mwadui, uliofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Kagera.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
http://www.tff.or.tz/news/717-mchezo-wa-kirafiki-kuchangia-rambirambi-msiba-wa-ismail-khaflan

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni