Mkuu wa Mkoa wa Ruwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen Zelote amewaagiza wakuu wa ke wa wilaya kwa kushirikiana na Halmashauri zao pamoja na wananchi kuwa na kiwanda angalau kimoja ili kutekeleza kauli mbiu ya maadhimisho miaka 55 Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vitendo.
Ameyasema hayo wakati alipomaliza kupanda mti kama ishara ya maadhimisho ya siku ya uhuru yaliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na watumishi wote wa ofisi yake.
Amewataka watumishi wote kila mmoja kuwa na mti wake ambao atauhudumia hadi kukua kwa mti huo, hii ikiwa ni mwanzo wa kampeni ya upandaji miti ili kuuokoa Mkoa wa Rukwa kugeuka kuwa jangwa.
Katika kutekeleza Kauli mbiu ya siku ya Uhuru wa Vitendo Mkuu wa Mkoa amezitahadharisha Halmashauri hasa idara ya ardhi, elimu, afya na mahakama juu ya kukithiri kwa rushwa.
"Tunajua kwamba rushwa ni kirusi kwa haya maendeleo ambayo serikali yetu imepania kuyaleta, hatutakubali yawepo," Mkuu wa Mkoa alisisitiza.
Pia amewataka wananchi kuwa huru kuitumia taasisi ya kupambana na rushwa katika kuripoti mtukio mbalimbali yenye harufu ya rushwa na kusisitiza kuwa wananchi wasitoe taarifa baada ya rushwa.
"Wananchi wasitoe taarifa baada ya rushwa maana aliyetoa na aliyepokea wote ni wahalifu, kwa maana hiyo tuhakikishe tunatoa taarifa za vitendo vya rushwa mapema," Mkuu wa Mkoa alifafanua.
Imetoewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
Ofisi ya Habari Mkoa wa Rukwa.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni