Bingwa wa ngumi wa dunia Mmarekani
Terence "Bud" Crawford amehukumiwa kwenda jela siku 90
kutokana na kuhusika na ugomvi uliotokea kwenye duka la bodi za
magari.
Jaji amemuamuru Crawford, 29, kuwa
chini ya uangalizi kwa miaka miwili na kufanya kazi za kijamii kwa
saa 120.
Crawford ametiwa hatiani kwa tabia
zisizofaa na kusababisha uharibifu wa mali mwezi Aprili huku Omaha,
Nebraska, wakati gari lake lilipokuwa linapigwa rangi.
Kifungo chake hiyo kimekuja baada ya
kupita siku tano tu, baada ya kumshinda John Molina na kutetea
mikanda ya WBC na WBO.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni