Bournemouth imeiduwaza Liverpool
baada ya kutokea nyuma na kuibuka na ushindi wa magoli 4-3 ikiwa ni
ushindi wake wa kwanza dhidi ya Liverpol katika mchezo wa kuvutia wa
Ligi Kuu ya Uingereza.
Bournemouth ilipambana baada ya
kulala magoli 2-0 katika nusu ya kwanza ya mchezo, na kisha 3-1 ikiwa
zimebakia dakika 15 na kumaliza mchezo huo kwa kuibuka na ushindi kwa
goli la dakika 93 la Nathan Ake.
Katika mchezo huo Sadio Mane
aliifungia Liverpool goli la kwanza na kisha kuongeza la pili kupitia
kwa Divock Origi kabla ya Callum Wilson kuifungia Bournemouth lakini
baadaye Emre Can akafunga goli la tatu.
Ryan Fraser aliifungia Bournemouth
goli la pili, likiwa goli lake la kwanza katika ligi kuu, kisha beki
wa kati Steve Cook kuisawazishia timu hiyo na Nathan Ake kufunga goli
la nne la ushindi.
Sadio Mane akipiga mpira uliomzunguka kipa Boruc na kisha kuupachika wavuni
Mchezaji mwenye asili ya Kenya Divock Origi akiangalia mpira alioupiga ukielekea kujaa wavuni
Nathan Ake akifunga goli la nne lililoizamisha Liverpool katika mchezo huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni