Cristiano Ronaldo amefunga magoli
matatu 'hat trick' na kuisaidia Real Madrid kutwaa kombe la klabu
bingwa dunia kwa ushindi wa magoli 4-2 dhidi ya Kashima Antlers.
Ronaldo alifunga goli moja kwa
mkwaju wa penati na kisha kutupia mengine mawili katika dakika za
nyongeza za michezo.
Karim Benzema alikuwa wa kwanza
kufunga goli katika mchezo huo, lakini Gaku Shibasaki akaisawazishia
Kashima, na kisha katika kipindi cha pili Shibashaki akafunga la
pili.
Cristiano Ronaldo akifunga goli kwa shuti la penati
Gaku Shibasaki akiifungia Kashima goli katika mchezo huo wa fainali
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni