Nyota wa soka Cristiano Ronaldo
ameonyesha kusikitishwa na hali ngumu ya maisha wanayokabiliana nayo
watoto katika taifa lililogubikwa na vita la Syria, katika video yake
aliyoiweka kwenye mitandao ya jamii.
Nyota huyo wa Real Madrid na Ureno
ametoa fungu nono la fedha kusaidia huduma za dharura mjini Aleppo,
ikiwemo msaada wa chakula, nguo na matibabu kwa familia nchini Syria
kupitia shirika la Save the Children.
Ronaldo amenukuliwa akisema “Hii
ni kwa ajili ya watoto wa Syria, tunajua mmekuwa mkitaabika mno, mimi
ni mtu maarufu katika soko lakini nyinyi ni mashujaa, tunawajali mno,
nami nipo nanyi”.
Cristiano Ronaldo akiongea huku ameshika kifua kuonyesha kuguswa na mateso ya watoto wa Aleppo
Mmoja wa watoto wa Aleppo akiwa ameokolewa kutoka kwenye jengo lililoshambuliwa kwa mabomu wakati wa mapigano
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni