Muigizaji filamu Carrie Fisher,
ambaye aliigiza kama Princess Leia katika filamu ya Star Wars, yupo
katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kupatwa na shambulizi la
moyo akiwa kwenye ndege.
Kaka wa muigizaji Fisher, 60,
amesema dada yake alipatwa na shambulizi la moyo angani dakika chache
kabla ya kumaliza safari yake ya kutokea London Uingereza kuja Los
Angeles Marekani.
Abiria walijaribu kumpa msaada wa
kwanza na ndege hiyo ilipotua alikimbizwa hospitali, kaka yake Todd
amesema kwa sasa Fisher yupo katika chumba cha wagonjwa mahututi
Jijini Los Angeles.
Carrie Fisher akipromoti kitabu chake cha The Princess Diarist
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni