.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 12 Desemba 2016

DIEGO COSTA AIREJESHA CHELSEA KILELENI MWA LIGI KUU YA UINGEREZA

Timu ya Chelsea imerejea tena kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza na kufikia idadi ya ushindi katika michezo tisa mfululizo, wakati Diego Costa akifunga goli pekee dhidi ya West Brom katika dimba la Stamford Bridge.

Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Hispania, Costa alitumia vyema kosa la kusita kwa Gareth McAuley katika dakika ya 76 ya mchezo huo na kuuwahi mpira kisha kupiga shuti la kuzungusha lililojaa wavuni.
  Diego Costa akipiga mpira wa kuzungusha uliojaa wavuni na kumshinda kipa wa West Brom
                             Diego Costa akishangilia baada ya mpira alioupiga kujaa wavuni

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni