Kiungo wa Manchester United Henrikh
Mkhitaryan atakuwa nje ya uwanja hadi Boxing Day baada ya kuumia enka
hapo jana katika mchezo ambao Manchester United ilishinda goli 1-0
dhidi ya Tottenham.
Kiungo huyo raia wa Armenia ambaye
ndiye aliyefunga goli hilo pekee katika mchezo huo alifanyiwa
madhambi na beki wa kulia Danny Rose na kulazimika kutolewa nje ya
uwanja.
Kocha wa Manchester United Jose
Mourinho amesema Mkhitaryan hajaumia sana, hivyo hahitaji kufanyiwa
upasuaji na anatarajia kushuka dimbani siku ya Boxing Day.
Danny Rose akimfanyia madhambi Enrikh Mkhitaryan iliyopelekea kuumia enka
Kocha Jose Mourinho akipiga shuti hewa baada ya kushikwa na midadi



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni