Magoli yaliyofungwa na Dimitri Payet
na Michail Antonio yameanika uzaifu wa beki ya Liverpool, wakati West
Ham ikijikwamu kutoka kwenye mstari wa kushuka daraja kwa kuambulia
sare ya magoli 2-2 katika dimba la Anfield.
Baada ya kufungwa magoli 4-3 na
Bournenouth wiki iliyopita, Liverpool ilijikuta ikifungwa magoli
mawili katika kipindi cha kwanza tu cha mchezo yaliyofungwa na Payet
na Antonio.
Katika mchezo huo Liverpool ilipata
goli la kwanza kupitia kwa Adam Lallana katika dakika ya tano ya
mchezo , na kisha kupata goli la kusawazisha kupitia kwa Divock Origi
katika kipindi cha pili.
Dimitri Payet akipiga kiufundi mpira wa adhabu ulioenda kujaa wavuni
Mshambuliaji mwenye asili ya Kenya Divock Origi akiifungia Liverpool goli la kusawazisha



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni