Timu ya Arsenal imepoteza nafasi ya
kuwea kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya Everton kutokea
nyuma na kupata ushindi wa magoli 2-1.
Arsenal ambao walikuwa wameshinda
michezo yao mitatu iliyopita, walipata goli la kwanza kupitia kwa
mpira wa adhabu uliopigwa na Alexis Sanchez na kumgonga beki Ashley
Williams.
Everton walisawazisha goli hilo
kabla ya mapumziko kupitia kwa Seamus Coleman akiunganisha krosi
murwa ya Leighton Baines. Beki Williams alifunga goli la pili kwa
mpira wa kichwa.
Mpira wa kichwa uliopigwa na beki Ashley
Williams ukijaa wavuni na kuandika goli la pili la Everton
Olivier Giroud akifuta machozi ya machungu ya kipigo
Katika mchezo mwingine Timu ya
Leicester City imejikuta ikipata kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa
wenyeji wao AFC Bournemouth goli lililofungwa na Marc Pugh mnamo
dakika ya 34.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni