Kocha wa Manchester City, Pep
Guardiola, amesema kuwa hajui iwapo atapatiwa muda anaohitaji kuijenga
timu yenye mafanikio katika dimba la Etihad Stadium.
Kipigo kutoka kwa Leicester City
jumamosi, kilikuwa ni kipigo cha pili mfululizo katika Ligi Kuu ya
Uingereza wakinolewa na Guardiola.
Manchester City wapo nyuma ya vinara
Chelsea kwa pointi saba na wameshinda michezo minne kati ya michezo
yao 15 katika michuano yote.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni