.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 30 Desemba 2016

KLABU YA CHINA YAMTEGA CRISTIANO RONALDO, MWENYEWE ACHOMOA

Mshambuliaji nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ameingia katika anga za wachezaji wanaowania na klabu za Ligi Kuu ya China na wakala wake Jorge Mendes amebainisha dau nono la kushangaza alilotengewa.

Kwa mujibu wa wakala huyo Ronaldo ameahidiwa mkataba wa malipo ya paundi milioni 1.6 kwa wiki, kutoka klabu mmoja ambayo haijatajwa ya China, na ipo tayari kuilipa Real Madrid ada ya uhamisho ya rekodi ya paundi milioni 260.

Hata hivyo inaonekana kuwa fedha si kila kitu kwa mchezaji huyo bora wa dunia, ambapo wakala wake Mendes amesema Ronaldo amekataa ofa hiyo nono ya kumg'oa real Madrid ili kwenda kwenye klabu ya China.
           Carlos Tevez yeye ameshatua China kusakata soko kwa malipo ya paundi 615,000 kwa wiki
        Oscar naye kung'oka Chelsea Januari kwenda China kwa ada ya paundi milioni 60

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni