Kocha wa Manchester City Pep
Guardiola ameomba radhi kwa timu yake kuhusika katika ugomvi
uliomfanya Sergio Aguero na Fernandinho kutolewa nje katika mchezo
ambao walifungwa 3-1 na Chelsea.
Katika mchezo huo jana Chelsea
walipigana kiume baada ya kufungwa goli moja na kuibuka na ushindi wa
nane mfululizo uliowafanya wakae kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza
wakiongoza kwa tofauti ya pointi ya pointi nne.
Sergio Aguero alijikuta akitolewa
nje kwa kadi nyekundu kwa kumshambulia beki David Luiz, huku mchezaji
mwenzake Fernandinho naye pia akionyeshwa kadi nyekundu kwa kugombana
na Cesc Fabregas.
Sergio Aguero akibaki na mshangao baada ya kupewa kadi nyekundu kwa kugombana na David Luiz
Fernandinho akisinikizwa kutolewa nje ya uwanja baada ya kukwaruzana na Cesc Fabregas
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni