Timu ya Liverpool imepunguza pengo
na kinara wa Ligi Kuu ya Uingereza Chelsea kuwa pointi 6 na kupanda
hadi katika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi baada ya kuifunga
Stoke City magoli 4- 1.
Stoke City ilikuwa ya kwanza
kuifunga Liverpool kupitia kwa Jon Walters lakini Liverpool walijibu
mapigo kupitia kwa Adam Lallana na Roberto Firmino ambao walifunga
magoli hayo kabla ya mapumziko.
Liverpool iliongeza goli la tatu
kupitia Giannelli Imbula aliyejifunga kwa kutumbukiza mpira wa krosi
ya Divock Origi na kisha Daniel Sturridge, alifunga goli lake la
kwanza la Kigi Kuu ya Uingereza kwa msimu huu.
Giannelli Imbula akijifunga kwa mpira wa krosi ya Divock Origi
Daniel Sturridge akimzungusha kipa wa Stoke City na kufunga goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni