Makosa ya mfululizo ya kiusalama
yamepelekea kumuacha mhamiaji hatari kutoka Tunisia kuwa huru na
kufanya shambulizi la kutumia lori Jijini Berlin katika soko la
Krismasi.
Kikosi cha Usalama cha Ujerumani
kinawakati mgumu wa kujibu maswali baada ya kubainika mtuhumiwa huyo
Anis Amris alikuwa na rekodi za uhalifu na alipaswa kurejeshwa kwao
miezi kadhaa iliyopita.
Amris, 24, ambaye sasa anasakwa na
limetangazwa donge nono la Euro 100,000 kwa atakayefanikisha
kukamatwa kwake, alikuwa chini ya uangalizi kwa miezi kadhaa tangu
2015.
Lori lililotumika kufanya mauaji ya watu 12 na kujeruhi wengine Jijini Berlin
Baadhi ya wahamiaji wakiweka maua katika eneo la tukio kuomboleza watu waliouwawa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni