Mamlaka nchini Nigeria imekamata
tani 2.5 za mchele wa plastiki uliokuwa umeingizwa kimagendo na
wafanyabiashara wasiowaaminifu nchini humo.
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato wa Lagos
Haruna Mamudu amesema mchele huo feki ulikuwa unatarajiwa kuuzwa
wakati wa Sikukuu.
Amesema kuwa mchele huo ulikuwa kama
gundi baada ya kuchemshwa, na kuongeza kuwa ni Mungu tu anajua nini
kingetokea iwapo watu wangeula.
Haijabainika mara moja mchele huo
umetokea wapi, ingawa mchele wa plastiki ulibainika nchini China
mwaka jana.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni