.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 15 Desemba 2016

MAHAKAMA YAMFUTIA MASHTAKA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA UVCCM ARUSHA ,WAKATI HUO HUO JESHI LA POLISI LAMSHIKILIA

Katikati ni aliyewai kuwa mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya akiwa anatoka mahakamani (picha na
maktaba)

 
Na Woinde Shizza,Arusha

Mahakama ya hakimu mkazi mkoani Arusha imefuta kesi iliyokuwa inamkabili aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Uvccm mkoani hapa Lengai Ole Sabaya baada ya upande wa Jamhuri kusema kuwa haitaki kuendelea na kesi hiyo.

Hakimu aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo Gwan'twa Mwangoka amesema kuwa shauri hilo lililetwa na serikali mahakamani hapo,hivyo mahakama imeona haja ya  kuendelea na shauri hilo.

Awali wakili upande wa Jamhuri Grace Makidenya aliwasilisha ombi mahakamani hapo la kuiomba mahakama kuiondoa kesi hiyo.

Kwa  upande wake wakili anayemtetea Sabaya amesema kuwa ipo mamlaka
anayokuwa nayo DPP kuondoa shauri mahakamani  hivyo kesi iliyokuwa
inamkabili imefutwa hivyo hakuna kesi inayomkabili tena.

Wakati huohuo Baada ya kufutiwa kesi na  mahakama Lengai Ole Sabaya alikamatwa tena na polisi ,mwandishi wa habari hizi alifanya
jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi mkoani hapa Charles Mkumbo
ili aweze kuzungumzia sakata la kukamtwa kwa Sabaya,Kamanda alisema kuwa  hiyo ni teknikali za kisheria bali kesi ni hiyo hiyo na jeshi la polisi
linafanya taratibu zao na zikikamilika watamrudisha tena mahakaman.

Miezi  kadhaa iliyopita aliyekuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi ‘UVCCM’ Arusha, Lengai Ole Sabaya alishtakiwa kwa kosa la
kujifanya ofisa usalama wa Taifa na kughushi kitambulisho cha usalama wa
 taifa. 

Kesi hiyo imetolewa maaamuzi na mahakama ya hakimu mkazi
 Arusha leo December 14 2016 ambapo imemuachia huru Lengai Ole Sabaya
baada ya upande wa Jamhuri kusema hawana nia ya kuendelea na kesi
hiyo

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni