Manchester United imetinga kirahisi
nusu fainali ya kombe la EFL, baada ya kuichakaza West Ham kwa magoli
4-1, huku kocha wao akitumikia adhabu ya kufungiwa mechi moja.
Katika mchezo huo Zlatan Ibrahimovic
alikuwa wa kwanza kufunga goli katika dakika ya pili tu ya mchezo
kabla ya kinda wa zamani wa United, Ashley Fletcher kusawazisha goli
hilo.
Anthony Martial alifunga goli la
pili la Manchester United mara tu baada ya kuanza kipindi cha pili
akiunganisha pande alilopigiwa na Henrikh Mkhitaryan.
Martial tena akaufunga goli la tatu
kufuatia krosi ya chini iliyopigwa na Antonio Valencia kufuatia
shambulizi lililopangwa vizuri, kabla ya Ibrahimovic kufunga goli la
nne.
Zlatan Ibrahimovic akielekea kufunga goli la kwanza katika mchezo huo
Zlatan Ibrahimovic licha ya kufunga goli hilo alikumbana na dhahama hii
Anthony Martial akifunga goli katika mchezo huo wa jana usiku




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni