Timu ya Southampton imefanikiwa
kutinga nusu fainali ya kombe la EFL kwa mara ya kwanza tangu mwaka
1987, kufuatia kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Arsenal.
Magoli kutoka kwa Jordy Clasie
ambaye ni goli lake la kwanza kwa klabu yake na la Ryan Bertrand
yaliipa Southampton ushindi wa kwanza dhidi ya Arsenal katika msimu
huu.
Meneja Arsene Wenger, ambaye
hajawahi kushinda kombe hilo alifanya kosa la kuwapumzisha wachezaji
wake 10 muhimu, kosa ambalo lilimgharimu.
Jordy Clasie akiachia shuti na kufunga goli la kwanza
Ryan Bertrand akifunga goli la pili la Southampton



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni