Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto aliyevaa kofia) akiwa na Katibu wa Timu ya Miembeni, Simai Mwalimu wakiingia ndani ya Uwanja wa Amani, Zanzibar kwa ajili ya kushuhudia timu hiyo inayotoka katika Jimbo la Masauni, ikipambana na Timu ya Taifa Jang’ombe katika mzunguko wa Ligi Kuu visiwani humo. Picha na MOHA.
Mchezaji
wa Timu ya Miembeni akipiga mpira kichwa akimtoka mpinzani wake wa Timu
ya Taifa Jang’ombe katika mechi ya Ligi Kuu Zanzibar iliyofanyika
katika Uwanja wa Amani na Timu hizo zilitoka sare kwa kufungana goli
moja kwa moja. Picha na MOHA
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiwa na Katibu wa Timu ya Miembeni, Simai Mwalimu wakiangalia wachezaji wa Timu ya Miembeni (hawapo pichani) ilipokuwa inafanya mashambulizi dhidi ya Timu ya Taifa Jang’ombe katika mzunguko wa Ligi Kuu ya Zanzibar zinazofanyika katika Uwanja wa Amani, mjini Unguja. Timu hizo zilitoka sare kwa kufungana goli moja kwa moja. Picha na MOHA.
Mashabiki wa Timu ya Miembeni wakishangilia wakati timu yao ilipokuwa imeifunga goli moja, Timu ya Taifa Jang’ombe, katika mashindano yaliyofanyika katika Uwanja wa Amani, Zanzibar. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) alihudhuria timu hizo zikipambana katika mzunguko wa Liki Kuu visiwani humo. Picha na MOHA.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa kofia) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Timu inayocheza Ligi Kuu, Miembeni Club pamoja na viongozi wao kabla ya timu hiyo kuanza kucheza na Timu ya Taifa Jang’ombe. Timu hiyo inatoka katika Jimbo la Masauni, ambapo aliwasili uwanjani hapo kwa lengo la kuwahamasisha wachezaji hao watoke na ushindi. Picha zote na MOHA.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni