Timu ya Leicester City ambayo tayari
imefuzu hatua ya mtoano katika Ligi ya Mabingwa Ulaya imejikuta
ikipata kipigo cha aibu cha magoli 5-0 kutoka kwa FC Porto katika
mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi.
Timu hiyo iliyoshuka dimbani baada
ya kuwa na uhakika wa kuwa ishasonga mbele katika kundi lao la G,
kocha wake Claudio Ranieri alifanya mabadiliko ya wachezaji kumi
ambayo yalimgharimu.
Timu ya Porto ambayo ilikuwa
inahitaji kushinda ili isonge mbele ilipata magoli yake kupitia kwa
Valente Silva, Jesus Corona, Yacine Brahimi, Silva akafunga tena kwa
penati na kisha Teixeira da Silva kufunga la tano.
Valente Silva akiangalia mpira wake wa kichwa alioupiga ukitinga wavuni
Jesus Corona akiwa amepiga mpira uliojaa wavuni na kuandika goli la pili
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni