Marco Reus amefunga goli la
kusawazisha katika dakika 88, na kuipatia Borussia Dortmund sare ya
magoli 2-2 dhidi ya Real Madrid, na kuihakikishia kumaliza kinara wa
kundi F katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Katika mchezo huo mshambuliaji
Mfaransa Karim Benzema alifunga magoli yote mawili la kwanza katika
kipindi cha kwanza na la pili kipindi cha pili na kuifanya Real
Madrid kuonekana kuutawala mchezo huo.
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund
Pierre-Emerick Aubameyang alichomoa goli la kwanza katika dakika ya
60, kabla ya Marco Reus kufanya mchezo huo umalizike kwa sare.
Karim Benzema akifunga bonge la goli kwa kuruka kichwa cha nguvu
Pierre-Emerick Aubameyang akifunga goli la kwanza la Dormund
Marco Reus akifunga goli la kusawazisha akimpoteza kipa Keylor Navas




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni