Timu ya Tottenham Hotspur
imefanikiwa kufuzu kutinga hatua ya mtoano katika Ligi ya Mabingwa
Ulaya baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya timu ya CSKA
Moscow ya Urusi.
Spurs, ilikuwa inahitaji kuepuka
kipigo ili kumaliza katika nafasi ya tatu katika kundi F, ilikuwa ya
kwanza kufungwa goli na Alan Dzagoev lakini goli hilo lilisawazishwa
na Dele Alli.
Harry Kane alifunga goli la pili,
kabla ya goli kipa wa CSKA, Igor Akinfeev kuizawadia Spurs goli kwa
kuuelekezea ndani ya goli lake mpira wa kichwa uliopigwa na Alli
wakati akijaribu kuuokoa.
Dele Alli akipiga mpira uliozaa goli la kwanza la Tottenham
Mshambuliaji Harry Kane akifunga goli la pili la Tottenham



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni