.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 30 Desemba 2016

MCHEZA TENESI SERENA WILLIAMS ACHUMBIWA NA ALEXIS OHANIAN

Serena Williams ametua New Zealand na kushuka dimbani kucheza tenesi, baada ya kutangaza kuchumbiwa na muanzilishi wa mtandao wa kijamii Reddit, Alexis Ohanian, kwa kutumia mashari matamu.

Nyota huyo wa tenesi duniani jana amebainisha kuwa rafiki yake huyo wa kiume kwa muda wa miaka miwili sasa Ohanian, alimuomba akubali kumchumbia baada ya safari ya kushtukiza aliyompeleka Jiji Roma.

Williams, 35, alifichua taarifa hizo kupitia mtandao wa Reddit kwa kutuma shairi 'Katika meza ile ile tuliyokutana bila ya kudhamiria/ Hivi sasa amepanga tukutane/ Kwa kudhamiria/ Akapiga magoti/ Akasema maneno manne/ Nami nikasema ndio.'
                    Serena Williams akivuta pete yake ya uchumba kwenye kidole chake

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni