Muigizaji nyota wa filamu wa
Marekani Charlie Sheen amebainisha kuwa amepona kabisa maambukizi ya
virusi vya Ukimwi baada ya kutumia dawa ya sindano iliyokuwa
inafanyiwa majaribio ya PRO-140.
Muigizaji huyo amekuwa akitumia dawa
hiyo iliyokuwa kwenye majaribio tangu mwaka 2016, amebainisha kuhusu
kutoishi tena Virusi vya Ukimwi katika siku ya Ukimwi, wakati
maafisa wa afya duniani wakisherehekea mafanikio yaliyofikiwa katika
tafiti za Ukimwi.
Kwa kipindi chote hicho Sheen
alikuwa akichomwa sindano moja ya dawa ya PRO-140 kila wiki, na
jumanne wiki hii alipewa taarifa na mkuu wa majaribio ya dawa hiyo
kuwa vipimo vinaonyesha hakuna tena virusi vya Ukimwi mwilini mwake.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni