Na Woinde Shizza ,Arusha
Idara ya uhamiaji imetakiwa kuhakikisha wanadhibiti ongezeko la wageni ,kwa kudhibiti uingiaji holela wa wageni kutoka nje ya nchi.
Hayo yamebainishwa na Waziri mkuu Kassim Majaliwa wakati akiongea na watumishi wa Serikali wote wa halmashauri zote zilizopo ndani ya jiji la Arusha ambapo alisema kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la wageni ambao wanaingia nchini bila vibali huku wengine wakiwa hawana shughuli ya msingi yakufanya.
Alisema serikali imepanga bajeti ya wananchi kulingana na idadi ya wananchi wao ,sasa wanapo kuja wananchi kutoka nje bila sababu ya msingi na wanaoingia kiholela wanaingizia shida serikali pamoja na wananchi kwa ujumla
Alisema kuwa ni wajibu taasisi ya uhamiaji kuhakikisha wanakagua wageni wote wanaoingia na sababu gani na kuhakikisha anayeingia, kwani pia kumekuwepo na silaha nyingi zinazoingia kiholela kutoka nchi za nje hivyo ni wajibu wa taasisi hii kuhakikisha wanaoingia Wapo salama.
"Sasa hivi hawa wageni wakiingia waulizwe wanakuja kufanya nini kama ni kutalii walipie ada na uhamiaji wawapangie watakaa siku ngapi ,kama anaingia kwa ajili ya biashara apangiwe Siku za kukaa na pia hawa wanaokuja pia wachunguzwe wanakuja salama au ana mambo yake mabaya"alisema Majaliwa
Aidha aliwataka maafisa uhamiaji wote kuhakikisha wanaimarisha ulinzi katika mipaka yote ,pamoja na kupita kwenye nyumba zote za wageni ili wajirithishe kama kweli wote waliolala humo ni watanzania na kama sio watanzania je wana vibali vya kuishi na iwapo kama hawana hatua staiki zitatumika .
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni