.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 29 Desemba 2016

NGULI WA HOLLYWOOD DEBBIE AMFUATA BINTIE CARRIE ALIYEFARIKI DUNIA

Muigizaji mkongwe wa Hollywood Debbie Reynolds amefariki dunia jana baada ya siku moja kupita tangu kutokea kifo cha binti yake muigizaji Carrie Fisher.

Reynolds (84) ambaye alikuwa akiandaa maziko ya binti yake Fisher (60) alisikika akiiambia familia yake kuwa anataka kuwa na Carrie.

Carrie Fisher, alifariki dunia jumanne kutokana na matatizo ya moyo yaliyompata usiku wa Krismasi akiwa kwenye ndege akitokea London kuja Los Angeles.
Debbie akimtambulisha mtoto wake Carrie katika ulimwengu wa filamu hii ilikuwa mwaka 1958
                               Carrie Fisher akimbusu shavuni mama yake Debbie Reynolds

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni