Kiongozi wa Kanisa Katoliki Dunia
Papa Francis amesema kuwa maana hali ya Ukristo ni kujiondoa katika
kuhangaikia mno vitu vya kidunia.
Akiongea katika ibada iliyokuwa na
ulinzi mkali Jijini Vatican, Papa Francis ameelezea kuguswa na
mahangaiko wanayopata watoto katika maeneo mbalimbali duniani.
Pia alielezea watu wanaopatwa na
njaa, wahamiaji wanaopitia njia hatari pamoja na mashambulizi ya
mabomu katika mji wa Aleppo.
Waumini waliohudhuria ibada ya usiku
wa Krismasi jana katika Kanisa la Mt. Peter Basilica walilazimika
kukaguliwa na vifaa maalum, ili kuimarisha usalama.
Papa Francis akibusu sanamu la mtoto Yesu
Papa Francis akiwa amebeba sanamu la mtoto Yesu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni