Wizara ya Ulinzi ya Urusi, imesema
ndege ya jeshi lake ikiwa na watu 92 imeanguka kwenye Bahari Nyeusi.
Ndege hiyo ilitoweka kwenye rada,
dakika 20 baada ya kuruka kutoka hoteli moja huko Sochi, ambapo hadi
sasa mwili wa mtu mmoja umepatikana.
Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema
ndege hiyo ya Tu-154 ilikuwa imebeba wanajeshi, wanamuziki wa bendi
maarufu ya jeshi ya Alexandrov pamoja na waandishi wa habari.
Habari zaidi zinasema ndege hiyo
ilikuwa ikielekwa huko Latakia nchini Syria.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni