Magoli matatu yaliyofunga na Alexis
Sanchez, yameihakikishia Arsenal ushindi wa kishindo dhidi ya West
Ham katika dimba la London, na kuifanya ikwee hadi katika nafasi ya
pili ya msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Katika mchezo huo Mesut Ozil
alifunga goli la kwanza baada ya kosa la Angelo Ogbonna lililomfanya
Sanchez kuuwahi mpira na kutoa pande lililomaliziwa vyema na Ozil.
Sanchez alifunga goli safi la pili
na kisha kuongeza la tatu kabla ya Andy Carroll aliyeshuka dimbani
kwa mara ya kwanza tangu Agosti 18 kuifungia West Ham goli kwa mpira
wa kichwa.
Jahazi la West Ham lilijikuta
likizidi kuzama pale Alex Oxlade-Chamberlain alipofunga kwa umahiri
goli la nne la Arsenal, na kisha baadaye Sanchez akakamilisha karamu
hiyo ya magoli kwa mpira safi wa kuubetua juu.
Alexis Sanchez akiachia shuti lililojaa wavuni na kumshinda kipa wa West Ham
Alexis Sanchez akikamilisha goli lake la tatu katika mchezo huo kwa kuubetua mpira juu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni