Kapteni Sergio Ramos amefunga goli
la kusawazisha katika dakika za majeruhi, na kuongeza rekodi ya Real
Madrid kutokufungwa katika msimu huu, huku akiinyima Barcelona
ushindi katika mchezo wa kwanza wa El Clasico.
Mshambuliaji Luis Suarez alikuwa wa
kwanza kutikisa nyavu kwa mpira wa kichwa, wa adhabu uliopigwa na
Neymar na kuifanya Barcelona kuongoza katika dimba la nyumbani la Nou
Camp.
Hata hivyo Cristiano Ronaldo nusura
afunge goli kabla ya Ramos kufunga goli la mpira wa kichwa kufuatia
mpira wa adhabu uliopigwa na Luka Modric na kuifanya Real Madrid
kuambulia pointi.
Luis Suarez namba 9 mgongoni akiangalia mpira wa kichwa alioupiga ukijaa wavuni
Sergio Ramos akiruka juu kuupiga mpira kichwa na kusawazisha goli katika dakika za mwisho
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni