Makumi ya watu wanahofiwa kufa baada
ya moto kutokea kwenye pati ya muziki unaotumbuizwa live katika
ukumbi uliopo kwenye ghala moja huko Oakland, California.
Mamlaka za California zimethibitisha
vifo vya watu 9, lakini zimesema wanajiandaa na uwezekano wa
kuongezeka idadi ya vifo hadi kufikia watu 40.
Mkuu wa Kikosi cha zimamoto wa
Oakland, Teresa Deloche-Reed, amesema watu kati ya 50 hadi 100
wanasemekana walikuwamo kwenye ukumbi huo wakati moto ukitokea.
Picha inayoonyesha moja ya eneo la ndani la ukumbi huo ulivyokuwa kabla ya kuungua moto
Mmiliki wa ukumbi huo Derick Ion Almena amenusurika kifo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni