Idadi ya watu waliojikuta wakiwa
hawana makazi kufuatia kimbunga kikali kilichoikumba Indonesia siku
ya jumatano, imeongezeka na kufikia watu 43,000.
Wakala wa Taifa wa Kukabiliana na
Majanga, umesema ukubwa wa tatizo umeanza kubainika kwa sasa wakati
timu ya uokoaji ikifanikiwa kuyafikia maeneo yaliyoathirika.
Watu wapatao 100 wamekufa na wengine
wengi wamejeruhiwa baada ya kutokea tetemeko lenye ukubwa wa alama
6.5 katika mkoa wa Aceh.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni