Mshambuliaji Lionel Messi ameanza
mazungumzo na timu yake ya Barcelona kuhusiana na mkataba mpya, huku
mshambuliaji mwenzake Luis Suarez akitarajia kutia saini mkataba mpya
na klabu hiyo hadi 2022.
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa
Argentina Messi, 29, kwa sasa anamkataba na klabu hiyo hadi Juni
2018, na kocha wa Barca, Luis Enrique, amesema anafarijika kuwa
mazungumzo yanaendelea vizuri.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni