.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 6 Desemba 2016

WAKAGUZI WA NDANI WATAKIWA KUSIMAMIA UBORA WA MIRADI MIKUBWA YA UJENZI WA MIUNDOMBINU

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika (kulia), akimsikiliza Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt. Faraji Kasidi (kushoto) wakati akielezea mafanikio na changamoto zinazokikabili chuo hicho. Kushoto kwa Mkuu wa Chuo ni Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Bw. Mohamed Mtonga, Msaidizi wa Mkuu wa Chuo Dkt. Samwel Werema, Mkaguzi wa Ndani Mkuu Msaidizi– Ukaguzi Mamlaka za Mitaa Bw. Mwanyika Musa na Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Kiufundi Bw. Amin Mcharo
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika (kulia), akijibu hoja zilizotolewa na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt. Faraji Kasidi (kushoto) alipofika Ofisi Kuu ya Chuo hicho kabla ya kufungua mafunzo ya siku nne ya wakaguzi kutoka mikoa ya Kanda ya Kaskazini.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt. Faraji Kasidi aliyesimama akitoa utangulizi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo kwa wakaguzi wa Ndani kutoka Serikali za Mitaa na Sekretarieti za Mikoa. Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika, Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Mohamed Mtonga, Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Kiufundi Bw. Amin Mcharo na kulia kwa Kaimu Mkuu wa Chuo ni Mkaguzi wa Ndani Mkuu Msaidizi wa Serikali – Ukaguzi mamlaka za mitaa Bw. Mwanyika Musa.

Wakaguzi wa Ndani kutoka Serikali za Mtaa na Sekretarieti za Mikoa wakiwa kwenye mafunzo ya ukaguzi, Mgeni Rasmi katika mafunzo hayo ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika. Mafunzo haya yanafanyika katika ukumbi wa Chuo cha Uhasibu Arusha, mkoani Arusha.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika (aliyesimama) akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya wakaguzi wa ndani ambapo alisema mpaka sasa wakaguzi wa ndani 308 wamepata mafunzo hayo na wakaguzi 32 wameshafanya mafunzo hayo kwa vitendo.
Wakaguzi wa Ndani kutoka Serikali za Mitaa na Sekretarieti za Mikoa katika picha ya pamoja. Waliokaa ni Mgeni Rasmi na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika kulia kwake ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt. Faraji Kasidi, Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Kiufundi Bw. Amin Mcharo na kushoto kwake ni Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Mohamed Mtonga na Mkaguzi wa Ndani Mkuu Msaidizi wa Serikali – Ukaguzi mamlaka za mitaa Bw. Mwanyika Musa.
Mgeni Rasmi na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika (katikati) wakibadilishana mawazo na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt. Faraji Kasidi (Kushoto) na kulia ni Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Mohamed Mtonga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika akimsikiliza Mkaguzi wa Ndani Mkuu Msaidizi wa Serikali – Ukaguzi mamlaka za mitaa Bw. Mwanyika Musa ambapo alisema mafunzo hayo ni muhimu kwani yamelenga kuimarisha ukaguzi wa miradi mikubwa ili ujenzi wake ulingane na thamani ya fedha iliyotumika.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt. Faraji Kasidi akumfafanulia jambo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika.
 
Benny Mwaipaja, WFM, Arusha

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Doroth Mwanyika, amewataka wakaguzi wa ndani nchini kuhakikisha kuwa miradi mikubwa ya ujenzi wa miundombinu ikiwemo barabara na majengo yanajengwa kwa ubora unaolingana na thamani ya rasilimali fedha iliyotumika.

Bi. Mwanyika ametoa rai hiyo Jijini Arusha wakati akifungua mafunzo ya siku nne ya wakaguzi wa ndani kutoka Halmashauri za wilaya na Sekretarieti za mikoa iliyoko Kanda ya Kaskazini, Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara

Amesema kuwa wabunge na wananchi kwa ujumla wamekuwa wakilalamikia miradi mingi mikubwa ikijengwa chini ya kiwango na kuisababishia serikali hasara kubwa kutokana na usimamizi mbovu unaofanywa na mamlaka na idara za serikali wakiwemo wakaguzi wa ndani.

“Nina Imani kuwa mafunzo mnayoyapata ya namna ya kukagua ubora wa miradi mikubwa inayotumia fedha nyingi za serikali yatasaidia kuokoa fedha na kuifanya miradi inayojengwa idumu muda mrefu” aliongeza Bi. Mwanyika.

Kwa upande wake Mkaguzi wa ndani Mkuu wa Serikali Bw. Mohammed Mtonga, amesema kuwa kuanzishwa kwa mafunzo hayo yanayofadhiliwa kupitia mradi wa kuboresha Mifumo ya Fedha (PFMRP), yanatokana na mahitaji makubwa ya ujuzi wa namna ya wakaguzi wa ndani wanavyoweza kutambua ubora wa miradi mikubwa ya ujenzi inayotekelezwa hapa nchini kama inakidhi viwango.

“Wakaguzi hawa si wataalamu wa masuala ya ukandarasi lakini uwezo wanaojengewa ni pamoja na kupelekwa kwenye miradi mikubwa ya uejnzi ikiwemo barabaraba ambapo wataelekezwa namna ya kutambua miradi ambayo haikidhi viwango na kutoa ushauri kwa watoa maamuzi ili kuokoa fedha ya serikali isipotee” aliongeza Mtonga.

Wakaguzi wa ndani 302 kutoka Halmashauri na Sekretarieti za Mikoa nchini wamepatiwa mafunzo hayo ambapo pamoja na mafunzo ya nadharia, wakaguzi hao wa ndani wamefundishwa kivitendo namna ya kutambua miradi iliyojengwa chini ya viwango

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni