Mchezaji nyota wa zamani wa
Liverpool Rigobert Song amepigwa picha kwa mara ya kwanza tangu
apatwe na kiharusi wiki tisa zilizopita.
Nguli huyo wa Cameroon, amepigwa
picha akiwa amevaa fulana na timu ya chini ya umri wa miaka 21 ya
Southport, ameonekana kudhoofika licha ya kutabasamu akiwa amekaa
kitandani.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka
40, alipoteza fahamu kwa siku mbili mwezi Oktoba baada ya kuugua
akiwa Odza Jijini Yaounde, Cameroon.
Rigobert Song akiwa chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kupatwa na kiharusi
Rigobert Song akiwa anazungumza na rafiki yake baada ya kupata nafuu hivi sasa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni