.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 4 Januari 2017

BALOZI DR. KAMALA ATEMBELEA KISIMA CHA MAJI CHA KATA MABALE AMBACHO KIMEACHA KUTOA MAJI

Mkazi wa Kata Kilimilile akichota maji baada ya mradi wa kata Kilimilile kuanza kutoa maji. Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala ameshuhudia kuanza kazi kwa mradi huo na amewaomba wananchi kutunza mradi huo. Balozi Kamala anaendelea na ziara ya kukagua miradi ya maji Wilayani Missenyi.
Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye miwani) akizungumza na mwananchi wa kata Mabale aliyefika kuchota maji katika bwawa la maji la Akashwa lililo kata Mabale. Bwawa hilo limekauka kwa kiasi kikubwa kutokana na kukosekana mvua kwa muda mrefu. Balozi Kamala ametembelea pia mabwaya ya Nyankere na Lwoga ambayo yako hatarini kukauka kama mvua hazitanyesha ndani ya kipindi kifupi kijacho.
Mbunge wa Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala(aliyeshika kisima cha maji) akitazama kisima cha kata Mabale Wilayani Missenyi ambacho kimeacha kutoa maji. Balozi Kamala ameshauri Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Missenyi kukagua kisima hicho.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni