Timu ya Barcelona imeibuka na
ushindi wa magoli 5-2 dhidi ya Real Sociedad na kutinga nusu fainali
ya kombe la Copa de Rey kwa ushindi wa jumla wa magoli 6-2.
Barcelona ilipata goli lake la
kwanza kupitia kwa Denis Suarez aliyegongeana vyema pasi na Luis
Suarez na kisha baadaye Neymar akaangushwa na kuzaa penati
iliyofungwa na Lionel Messi.
Luis Suarez aliongeza goli la tatu
dakika moja tu kupita baada ya Juanmi kuifungia Real Sociedad goli la
kwanza na Da Silva aliifungia Sociedad goli la pili kabla ya Turan
kufunga goli la tano la Barcelona.
Denis Suarez akiachia shuti la umbali wa yadi 16 na kufunga goli la kwanza
Neymar akiwa amechezewa madhambi na beki Martinez na kusaidia kupatikana kwa penati
Luis Suarez akimalizia kilaini pande alilopewa na Lionel Messi na kufunga goli




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni