.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 27 Januari 2017

MANCHESTER UNITED YATINGA FAINALI KOMBE LA EFL LICHA YA KUFUNGWA

Timu ya Manchester United imefanikiwa kutinga fainali ya kombe la EFL ambapo itavaana na Southampton licha ya kufungwa magoli 2-1 na Hull City katika mchezo wao wa marudio wa nusu fainali hapo jana.

Kikosi cha Jose Mourinho kilikuwa kinaongoza kwa magoli 2-0 iliyoyapata katika mchezo wao wa awali kilishuka jana kikiwa kimefanya mabadiliko ya wachezaji watano katika dimba la KCOM Stadium.

Mchezaji Tom Huddlestone aliwapatiwa wenyeji goli la kwanza kwa mkwaju wa penati, lakini Paul Pogba akasawazisha kabla ya Oumar Niasse kufunga goli la pili akiunganisha pasi ya David Meyer na kusitisha rekodi ya Manchester United kutofungwa michezo 17.
                       Paul Pogba akifunga goli pekee la Manchester United katika mchezo huo
                                             Msenegali  Oumar Niasse akifunga goli la pili la Hull City

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni