.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 29 Januari 2017

BURKINA FASO YATINGA NUSU FAINALI YA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA

Timu ya Burkina Faso imefunga magoli mawili ya dakika za mwisho na kupata matokeo ya magoli 2-0 dhidi ya Tunisia na kutinga nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Mchezaji aliyetokea benchi Aristide Bance alifunga goli la kwanza kwa shuti la chini la mpira wa adhabu dakika tano tu tangu atokea benchi.

Prejuce Nakoulma aliihakikishia Burkina Faso ushindi kwa shambulizi la kushtukiza, baada wachezaji wote wa Tunisia kwenda kushambulia.

Kwa ushindi huo Burkina Faso itavaana na Morocco ama Misri katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo siku ya jumatano.
       Prejuce Nakoulma  akimzunguka kipa wa Tunisia na kwenda kufunga goli la pili 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni