Mchezaji wa Liverpool, Sadio Mane,
amekosa penati muhimu wakati Cameroon ikiifunga Segegal magoli 5-4
kupitia mikwaju ya penati na kutinga nusu fainali ya Kombe la Mataifa
ya Afrika.
Mane,ambaye ni mchezaji ghali wa
Afrika kuliko wachezaji wengine penati yake ilizuiliwa na kipa
Fabrice Ondoa, huku mchezaji wa Cameroon Vincent Aboubakar akifunga
goli la penati la ushindi.
Senegal iliyocheza vizuri katika
mchezo huo ilikuwa na nafasi kubwa ya kushinda katika muda wa
kawaida, ambapo shuti la Moussa Sow lilipaa juu na kuufanya mchezo
huo uliopigwa kwa dakika 120 kuishia bila goli.
Matokeo hayo yanatoa nafuu kwa
Liverpool ambayo ambayo imekuwa ikimkosa Mane, huku jana ikipata
kipigo cha kushtua cha magoli 2-1 kutoka timu ya Wolverhampton
Wanderers katika kombe la FA.
Sadio Mane akiwa amekaa chini akitafakari baada ya kukosa penati
Wachezaji wa Senegal wakiwa hawaamini kilichotokea baada mchezaji wao tegemeo Sadio Mane kukosa penati



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni