.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 15 Januari 2017

EVERTON SI YA MCHEZO MCHEZO YAIPIGA 4G MANCHESTER CITY

Everton imeonyesha mchezo mzuri na kuiduwaza Manchester City kwa kuipatia kipigo kikali cha magoli 4-0, ambacho ni pigo katika harakati za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Everton waliweza kudhibiti umiliki wa asilimia 71 wa Manchester City, kwa kutumia vyema nafasi nne kufunga goli kati ya sita walizopata.

Romelu Lukaku alifunga goli la kwanza kufuatia pande la Kevin Mirallas na kisha baadaye Lukaku akishirikiana vyema na Mirallas ambaye aliachia shuti na kufunga goli la pili.

Tom Davies aliibua shangwe katika dimba la Goodison Park baada ya kufunga goli katika sekunde chache tangu aingie dimbani kwa mara ya kwanza akicheza mchezo wa ligi kuu, na Ademola Lookman akafunga.
                        Romelu Lukaku akiwa ameachia shuti lililoandika goli la kwanza la Everton
Maumivu ya kichwa huanza taratibu: Silva akiwa ameshikilia kichwa akisikilizia maumivu ya kufungwa 
         Kocha Pep Guardiola naye mkono kichwani, kipigo si mchezo leo ni mwendo wa panadol tu

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni