.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 15 Januari 2017

PAMBANO LA JAMES DEGALE NA BADOU JACK LAMALIZIKA KWA SARE

Pambano la super-middleweight la mikanda miwili baina ya bondia Muingereza James DeGale na raia wa Sweden Badou Jack limemalizika jana usiku kwa sare yenye utata.

Jack aliangushwa chini katika raundi ya kwanza lakini alimaliza pambano hilo akiwa imara na kumuangusha chini DeGale katika raundi ya mwisho Jijini New York.

Jaji mmoja ametoa uamuzi wa kumpa bondia DeGale by pointi 114-112, lakini wengine wawili walitoa pointi 113-113, na kuwafanya mabondia hao kubakia na mataji yao.

Bondia aliyestaafu masubwi Floyd Mayweather, ambaye alikuwa ni promota wa Jack, amesema uamuzi huo wa majaji, ni mbaya kwa mchezo wa ngumu.
                                Bondia James DeGale akiwa amemuangusha bondia chini Jack Badou
                                  Bondia Badou Jack akiwa amemuangusha chini bondia James DeGale 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni